Friday, January 31, 2014

Kuwafanya Wagonjwa Kuwa Wanafunzi

(1 Yohana 3, Marko 2, Kumbukumbu la Torati 28, Luka 9)
Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.
Utangulizi: Je, ungependa washiriki waongezeke zaidi kanisani kwako? Huo ndio mjadala unaoendelea kanisani kwangu hivi sasa! Watu wana mawazo ya kufanya utandaaji, lakini mimi wazo langu ni kwamba “Hebu tufanye juhudi za kuwaponya wagonjwa!” Je, umewahi kufikiria kwamba hiyo ni njia nzuri ya kuwaleta washiriki wapya kanisani kwako? Hiyo ndio njia aliyoitumia Yesu, si ndio? Au, je, alitumia njia gani? Je, Yesu aliwaponya watu ili ayavute makundi makubwa ya watu kumsikiliza, au aliwaponya watu kwa sababu aliwahurumia? Endapo unawaponya watu ili kuwavutia watu wengine kuisikiliza injili, je, huko sio kuonesha huruma? Hebu tuzame kwenye somo letu la Biblia ili tuone kile tunachoweza kujifunza juu ya kukabiliana na ugonjwa!
I.                   Mioyo na Uponyaji
A.                Soma 1 Yohana 3:16-18. Wangapi kati yenu wanapendelea kuonesha upendo kwa maneno? (Kwa sababu gharama yake ni ndogo, hutumia muda mfupi, na kuna maumivu kidogo!)
1.                  Je, Biblia inatuasa kuwa tuonesheje upendo? (“Kwa matendo na kweli.”)
a.                   Je, kauli ya “kwa kweli” inamaanisha nini katika huu muktadha? (Inamaanisha kwamba kutenda jambo fulani kunafanya matendo yako ya upendo yawe ya kuaminika.)
B.                 Soma 1 Yohana 3:19-20. Je, inamaanisha nini kwa “mioyo yetu kutuhukumu?” (Inamaanisha kujisikia hatia.)
1.                  Je, Biblia inatuambia nini katika haya mafungu tuliyojifunza? (Tunatakiwa kuonesha upendo si kwa maneno tu. Tutajisikia vizuri kwa kuwasaidia watu walio wahitaji.)
C.                 Je, mafungu haya yanaashiria nini kwenye maswali niliyoyauliza kwenye utangulizi? Endapo tunaweza kufanya uponyaji kuwa sehemu ya uinjilisti kwa njia ya utandaaji, je tunapaswa kufanya hivyo? (Ndiyo! Bila kujali kama unafanya uponyaji ili kuvutia makundi ya watu kuisikiliza injili, au unawaponya wale ambao tayari wameshavutiwa na injili, unaonesha kujihusisha kwako kwenye pande zote mbili za wahusika – hali ya kiroho na ya kimwili.)
D.                Soma 1 Yohana 3:21-22. Je, umeuona uponyaji kanisani kwako?
1.                  Kama hujauona, je, fungu hili linaashiria nini? (Kwamba tunaweza kuuomba uponyaji.)
2.                  Je, ahadi hii ina masharti yoyote? (Inasema kuwa tunaweza kupokea jambo lolote tuliombalo endapo tunamtii Mungu.)


E.                 Soma 1 Yohana 3:23. Je, tunazungumzia utii wa aina gani? (Kumwamini Yesu na kuwapenda watu wengine. Hii inaashiria kuwa tunatakiwa kuyapa kipaumbele maombi kwa ajili ya uponyaji (kumwamini Mungu) kwa niaba ya watu maalum (kuwapenda wengine).)
F.                  Soma 1 Yohana 3:24. Je, tunakaaje ndani ya Yesu na Yesu anakaaje ndani yetu? (Hii ni rejea mahsusi ya Roho Mtakatifu kukaa ndani yetu na sisi kuishi maisha yanayoendana na matakwa ya Roho Mtakatifu. Hili ni jambo la muhimu sana.)
G.                Hebu tuwe wakweli kabisa kwa dakika chache. Jambo gani linafanya kuwasaidia watu wengine liwe na maumivu? Hivi punde tu nimesema kuwa kuwasaidia watu wengine kunatufanya tujisikie vizuri. Je, ni yote mawili?
1.                  Je, unaweza kubainisha nyakati ambazo ulijisikia vizuri kuwasaidia watu wengine na nyakati ambazo ulijisikia vibaya? Je, jambo gani linaleta utofauti? (Kutatua tatizo kwa mtu mwenye shukrani kunafanya mtatuzi wa tatizo ajisikie vizuri. Tatizo la kudumu lisilotatulika linalomhusisha mtu asiye na shukrani huleta maumivu/hukatisha tamaa kwa mtatuzi wa tatizo.)
2.                  Je, Yesu alishughulikaje na matatizo ya watu waliomwendea? (Alitatua matatizo yao mara moja. Hebu tuangalie mfano katika sehemu inayofuata.)
II.                Yesu na Uponyaji
A.                Soma Marko 2:1-3. Je, watu wanakuja kwa ajili ya kusikiliza neno au kwa ajili ya uponyaji? (Yote mawili. Lakini inaonekana kama vile watu wengi zaidi wanakuja kwa ajili ya kusikiliza maneno ya Yesu.)
B.                 Soma Marko 2:4. Endapo ungekuwa unazungumza na makutano, je, ungependa kumwona mtu akitoboa dari kwenye mahali ambapo unazungumza na watu?
1.                  Je, ungependa kuona mtu akishushwa kupitia katikati ya watu? (Litakuwa jambo la kuvuruga usikivu wa watu.)
C.                 Soma Marko 2:5. Je, Yesu anarejea imani ya nani? (Inaonekana kama anarejea imani ya kundi la watu waliomshusha, na sio tu imani ya yule mgonjwa, kwa kuwa kauli ya Yesu inasema, “imani yao.”)
1.                  Jiweke kwenye nafasi ya mmojawapo wa wale wasaidizi wanne. Je, Yesu anasema maneno ambayo ulikuwa unatarajia kuyasikia? (Hapana! Mwenzangu amepooza. Nisingekuwa na haja ya kumpitishia darini na kumshusha hadi chini kwa ajili ya kusamehewa dhambi. Ninataka Yesu amponye.)
a.                   Je, inawezekana kwamba Yesu anazungumzia dhambi ya kuingilia wasilisho/mazungumzo yake?
D.                Soma Yohana 9:1-3. Je, swali la wanafunzi linafunua nini juu ya fikra za watu kuhusu dhambi na ugonjwa? (Mambo yote mawili yanahusiana.)
1.                  Je,Yesu anafanya hitimisho juu ya hii imani maarufu? (Anafanya hivyo kwenye hili suala pekee. Hajibu kuwa, “Mnasema nini, hivi mmekuwa wendawazimu?” Badala yake, anasema kuwa hapa si dhambi za wazazi wala za mtoto zilizochangia kwenye tatizo.)
2.                  Je, unafikiria nini juu ya sababu aliyoitoa Yesu?
a.                   Kumbuka kisa cha Ayubu na marafiki wake? Marafiki wa Ayubu walimwambia Ayubu kuwa alikuwa akiteseka kwa sababu ya dhambi zake. Je, jibu analolitoa Yesu kuhusu mtu kipofu linahusika kwenye muktadha wa Ayubu? (Ndiyo!)


E.                 Hebu turejee kwenye kisa chetu juu ya mtu aliyepitishiwa darini. Soma Marko 2:6-8. Je, waandishi wako sahihi? (Ndiyo, Mungu ndiye anayesamehe dhambi.)
1.                  Kama waandishi wako sahihi, kwa nini Yesu anawauliza? (Kwa sababu hili ni suala tata kwa miaka mingi – je, Yesu ni Mungu?
F.                  Soma Marko 2:9-12. Hebu tupitie maswali tuliyoyaibua hapo awali. Kwa nini Yesu alitenda huu uponyaji? (Inaonekana sababu kubwa ni kuthibitisha kuwa yeye ni Mungu.)
1.                  Endapo tutamwomba Roho Mtakatifu awaponye watu ili tuweze kuwaleta watu kanisani, je, hiyo itakuwa sababu thabiti? (Tunataka kuwaongoa watu ili watambue kwamba Yesu ni Mungu.)
2.                  Je, ni sababu gani nyingine zinazoashiriwa kwa huu uponyaji? (Angalia tena Marko 2:5. Yesu alihamasishwa na imani yao.)
a.                   Je, jambo hili linatufundisha nini kuhusu mpango wa kutumia uponyaji ili kuiendeleza injili? (Tunatakiwa kuwa na imani. tunatakiwa kuiombea.)
b.                  Kutokana na kisa hiki, unadhani tunaweza kufanya hivi kanisani kwetu? Je, tungeweza kufanya uponyaji endapo tungekuwa na uwezo wa Roho Mtakatifu? (Fikra ya kawaida inaweza kuwa ni mtego. Angalia njia ya marafiki isiyo ya kawaida. Hawakumwambia rafiki wao, “Hatuwezi kufanya hivi leo, watu ni wengi sana.” Badala yake, mmoja wao alipendekeza, “Hebu tupande darini na tutoboe tundu analoweza kupita mtu ili tuweze kuingilia wasilisho la Yesu kwa kukuweka mbele yake. Nadhani Yesu atatupatia thawabu kwa jambo hili!” Hiyo ni imani, sio mantiki.)
G.                Soma Kumbukumbu la Torati 28:15 na Kumbukumbu la Torati 28:20-22. Je, watu walikuwa sahihi kufikiria kwamba kuna uhusiano kati ya dhambi na ugonjwa? (Ndiyo, kabisa. Ninaona angalao sababu tatu kuu za ugonjwa: a) Tunaishi kwenye dunia yenye dhambi; b) Kushindwa kwetu wenyewe; na, c) Kumpa Mungu utukufu. Mara nyingine sababu zote tatu zinaonekana kuhusika.)
III.             Uponyaji na Utandaaji
A.                Soma Luka 9:1-2. Kama kuna uhusiano kati ya dhambi na ugonjwa, je, “tunawaponya” watu kwa kuwaongoa? (Ndiyo!)
1.                  Je, hii ndio njia ya kuliendeleza kanisa? (Tunaonesha ubunifu wa fikra tunapoliendeleza kanisa kwa kusema kuwa endapo unamfuata Yesu utakuwa mwenye afya njema, na maisha yako yatakuwa bora.)


B.                 Mojawapo ya mambo mazuri kuhusu mimi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Regent ni kwamba walimu na wanafunzi wengi ni sehemu ya kile ninachokiita Ukristo wa “Utakatifu wa Kipentekoste.” Hawa ni Wakristo wanaochukulia suala la utii kwa Mungu na uwezo wa Roho Mtakatifu kwa umakini sana. Utagundua kwamba Luka 9:1 inawazungumzia wanafunzi “Kumi na Wawili.” Je, uponyaji ulitengwa kwa ajili yao au katika kipindi chao? (Soma Yohana 14:12-14. Fungu hili linasema kuwa “mambo makubwa” yanawezekana kwa “yeyote aniaminiye.” Katika mafungu machache yanayofuatia (Yohana 14:16-17) Yesu anaahidi kutupatia Roho Mtakatifu ili akae pamoja nasi. Uponyaji unawezekana kwa njia ya uwezo wa Roho Mtakatifu.)
C.                 Soma 1 Wakorintho 12:8-9. Je, hii inatufundisha nini? (Mambo mawili. Uponyaji ni karama ya Roho. Pili, Mungu ni mkuu (mwenye enzi). Anaamua ampatie nani karama na nani aponywe.)
D.                Soma Ufunuo 21:3-4. Je, hatma ya ahadi ya uponyaji ni ipi? (Wale watakaookolewa wataishi kwenye dunia itakayofanywa upya, mahali ambapo kifo, maumivu na ugonjwa vitakuwa ni mambo ya zamani. Sifa kwa Mungu!)
E.                 Rafiki, Mungu anaweza kukupatia karama ya Roho wa uponyaji, lakini hata kama hakukupatia, unao uwezo wa kuwaambia watu wengine habari za Yesu. Uhusiano na Yesu unatusaidia kuepuka kujiletea ugonjwa na unatupatia ahadi ya kuwa na dunia isiyo na dhambi na ugonjwa. Kwa nini usishiriki habari hizi na watu wengine leo?

Church History Timeline / Historia ya kanisa la kwanza


14 Augustus died on August 19. On September 17, the Senate in Rome decreed that Augustus Caesar was one of the gods, and it named Tiberius emperor. (If Luke 3.1 dates “the reign of Tiberius Caesar” from this year, his fifteenth year was 28/29 A.D.)
30, 33? Jesus was crucified and resurrected.

39/40 Philo of Alexandria (15/10 BC - 45/50) led an embassy of Jews from Alexandria to the emperor Caligula (37-41) in Rome. The Jews of Alexandria were then the subject of a Roman pogrom, which Philo and his companions hoped to end. Caligula, however, cut Philo off as he spoke. Philo later told his fellow ambassadors that God would punish Caligula, who was soon assasinated.

Philo was a theologian who sought to harmonize Jewish theology with Greek (largely Platonic) philosophy. Many ideas found in later Christian theology are present in Philo, though sometimes in a form unacceptable to the Church. Philo taught that Greek philosophy had been plagiarized from Moses. He believed that the Greek translation of the Old Testament (the Septuagint, dating from the third century BC) was divinely inspired. Philo referred to the Logos (the residence of the Platonic Ideas) as the first-begotten Son of God - though, in his view, the Logos was definitely below God, distinct from the Godhead. He interpreted the theophanies of the Old Testament as appearances of the Logos (as for the Fathers they were Christophanies). He stressed the allegorical interpretation of scripture, though this must be balanced. With the later Eastern mystical theologians, Philo discussed the incomprehensibility of God in essence, and how knowledge of God can be attained in an ecstatic state.

In some ways, Philo was more akin to the Gnostics and Manichaeans. For instance, like Plato, Philo viewed the body as the prison for the soul. This reveals a distinctly non-Christian view of matter.

41 Jerusalem expanded. New city walls were built, bringing the site of Jesus’ crucifixion within the city.

42James, the brother of John, was beheaded (Acts 12.2).

43 The emperor Claudius (41-54) conquered Britain.

Barnabas brought Saul to Antioch (Acts 11.25-26).

44 Death of Herod Agrippa I, King of Judea and Samaria (Acts 12.23).

45 The church in Antioch sent famine relief to the Christians of Judea by the hands of Saul and Barnabas (Acts 11.29).

47-49 First missionary journey of Saul and Barnabas (Acts 13-14).

49 According to the Roman historian Suetonius (70-122) in his The Twelve Caesars, Claudius “expelled the Jews from Rome since they rioted constantly at the instigation of Chrestus.”

49/50 The council of Jerusalem was held (Acts 15). As a result, Gentiles were not required to be circumcised.

Death of Helena, queen mother of the kingdom of Adiabene, a Jewish state in northern Mesopotamia. Adiabene was frequently allied with Persia in wars against Rome.

The emperor Claudius promoted the cult of the Great Mother (Magna Mater) of the Gods and her consort Attis. The two had been introduced into the Roman pantheon around 200 B.C.

50 Paul’s second missionary journey began, with Silas (Acts 15.40). Paul and Silas visited Philippi (Acts 16.11-40), meeting Lydia, the seller of purple, and being rescued from prison, with the consequent conversion of the Philippian jailor (Acts 16.33); Thessalonica, where there was a riot on their behalf (Acts 17.5); Boroea, where the Jews willingly examined the Old Testament prophecies of the Messiah (Acts 17.11); Athens, where Paul preached in the Areopagus (Acts 17.22-31); Corinth, where he met Aquila and Priscilla, refugees because of Claudius’ expulsion of the Jews from Rome (Acts 18.2); and Ephesus, Caesarea, and Jerusalem before returning to Antioch (Acts 18.22).

51 Paul wrote the epistles to the Thessalonians, from Corinth.

53 Paul’s epistle to the Galatians written from Antioch (?). Beginning of the third missionary journey. Paul in Ephesus, 53-55/56. (Acts 19)

55 Paul wrote 1 Corinthians, from Ephesus.

55/56 Paul departed Ephesus (Acts 20.1), visiting Macedonia and Corinth. 2Corinthians written from Macedonia.

57 Paul wrote Romans from Corinth. Departed Greece (Acts 20.3), and after passing through Troas (Acts 20.7-12), and preaching to the presbyters of the church in Ephesus (Acts 20.18-35), came to Jerusalem (Acts 21.17), ending the third missionary journey.

57-59 Paul imprisoned in Caesarea (Acts 23.33-26.32), under Felix and Festus.

60 Paul arrived at Rome (Acts 28.16).

61/62 Paul wrote the epistles entitled Philemon, Colossians, Ephesians and Philippians.

62 According to tradition, James the Just, bishop of Jerusalem, was killed in the temple by an angry mob, apparently struck in the head with a sledgehammer.

Tradition has it Bartholomew was martyred in Kalyana, a city state on the west coast of India, near modern-day Bombay. Bartholomew was skinned alive and crucified.

Paul tried and acquitted in Rome.

63-66 Paul traveled to Macedonia, Asia Minor, Crete, and possibly Spain. 1 Timothy and Titus written.

641st Persecution of Christians, under Nero. When Rome burned for six days, Nero (54-68) blamed the Christians. In 62, Nero had married Poppea Sabina, a proselyte to Judaism. Of Nero’s persecution, Tacitus wrote, “First Nero had self-acknowledged Christians arrested. Then, on their information, large numbers of others were condemned. ...Their deaths were made farcical. Dressed in wild animal’s skins, they were torn to pieces by dogs, or crucified, or made into torches to be ignited after dark as substitutes for daylight.” Suetonius was more succinct: “Punishments were also inflicted on the Christians, a sect professing a new and mischievous religious belief.”

A third century legend has it that Simon Magus (Acts 8.9-24) and St. Peter had confrontations in Rome. Simon, wishing to gain an advantage over Peter and to impress Claudius with his ability to fly, fell to his death from the top of the Roman Forum.

64 The church in Alexandria founded by St. Mark, the disciple of Peter.

64 Herod’s temple in Jerusalem completed. See 20 BC and 66.

66Jewish rebellion began and war between the Romans and Jews ensued. Jerusalem was taken in 70 and destroyed, as was Herod’s temple. Later, in the second century, Justin Martyr would teach that this destruction was the judgment of God upon a nation that had rejected its Messiah and failed to discern that, under the new dispensation, the temple sacrifices were abrogated.

67 Some date the book of Revelation to this year. Most place it toward the end of Diocletian’s reign (81-96).

Paul’s second trial in Rome. 2 Timothy written.

66 First known public reference to Mithraism in Rome. King Tiridates of Armenia visited Nero in Rome. To Nero he said, “I have come to thee, my god, to worship thee as I do Mithras.”

67/68 St. Paul martyred on the road from Rome to Ostia. Beheaded by the sword. About this same time St. Peter also martyred, crucified upside down.

69 According to tradition, St. Andrew was crucified in Patrae, on the Peloponnesus peninsula.

69Ignatius became bishop of Antioch in Syria.

69Polycarp, bishop of Smyrna, was born. He died in around 157. Irenaeus stated that Polycarp had known St. John at Ephesus. Polycarp was martyred and was noted for doing nothing to provoke the authorities, but waiting quietly for them to come arrest him. Irenaeus wrote, “Polycarp also was not only instructed by the Apostles, and conversed with many who had seen Christ, but was also by Apostles in Asia, ordained Bishop of the Church in Smyrna, whom I also saw in my early youth, having always taught the things which he had learned from the Apostles, and which the Church has handed down, and which alone are true.”

70 Near this date, R. Jochanan ben Zaccai founded a rabbinical school in Jamnia (Palestine).

Matthew and Mark’s gospels were probably written shortly after this year. Luke’s gospel may have been composed as late as 80.

72 Tradition has it Thomas was stabbed to death by Brahman priests in Mylapore, India.

79 According to tradition, Jude and Simon were torn apart by a Persian mob after this date. Simon had joined forces with Jude after a trip to Britain. Jude had been in Armenia.

80 The Coliseum at Rome opened.

90 The Jewish Synod of Jamnia established the Hebrew canon, the modern Protestant Old Testament. Esther, Ecclesiastes, the Song of Solomon, and Ezekiel were nearly left out of the canon, while Sirach was a strong but unsuccessful contender for inclusion. Rabbis at Jamnia also articulated the theory that every letter in the Hebrew has a meaning. It is thought by many that, as a natural consequence of this view of scripture, a standard text was chosen around this time and non-standard readings were suppressed.

The language of the early church was Greek, and the version of the Old Testament in use among both Christians and Jews of the diaspora was the Septuagint. The Septuagint contains books (sometimes termed “the Apocrypha”) not included in the Jamnian canon. As the Septuagint’s prophecies of the Messiah frequently were used polemically by Christians, the translation fell out of favor among the Jews. In time, non-Palestinian Jews accepted the decisions of Jamnia. New translations of the Old Testament scriptures were made based on the Jamnian standard text.

90 According to tradition, Philip was crucified upside down (like Peter) in Hierapolis, Asia Minor. (Some say that Philip the apostle and Philip the evangelist were two distinct individuals, and it was Philip the evangelist who was buried at Hierapolis.)

90 According to Hippolytus, Matthew died a natural death, in Hierees, Persia.

92Clement elected bishop of Rome. Served through 100. He wrote a letter to the Corinthian congregation which had deposed its old clergy and replaced them with new men. He asked that they retain the former clergy on the grounds that these stood in due succession from the apostles. “The Apostles knew through our Lord Jesus Christ that contentions would arise about the office of the Episcopate; and for this reason, being endued with perfect foreknowledge, they appointed those already mentioned, and handed down a succession, so that when they should depart, other approved men should succeed to their ministry.” (~97.)

In 2 Clement, which may be a second century document, it is written, “Brethren, we ought so to think of Jesus Christ as of God ... for if we think meanly of him, we shall hope only to receive some small things from him.”

93 2nd Persecution of Christians, under Domitian (81-96). The apostle John banished to Patmos.

Flavius Josephus (37/38-100) published his Antiquities of the Jews. Book 18 refers to Jesus Christ. Scholars believe the statement was tampered with by Christians at a later date, because it refers to Christ as divine. Josephus had been a leader of troops against the Romans in Galilee during the war (66-70). When captured, he predicted that Vespasian would become emperor, a move that saved his life. Josephus wrote a history of the war, and, because of the favoritism he received from the Roman emperors, was detested by his fellow Jews as a traitor.

100 Around this time St. John died at Patmos. (Eusebius, Irenaeus and Clement of Alexandria agree that John lived into the reign of Trajan, which began in 98.) The Didache, written in this era, indicates worship was on Sunday: “Assemble on the Lord’s day, and break bread and offer the eucharist; but first make confession of your faults, so that your sacrifice may be a pure one.” Note also the implication that the communion was regarded as a sacrifice.

100? Around this time the heretic Cerinthus flourished. He taught that the world was made, not by God himself, but by a lower being. He also claimed that Jesus was simply the natural son of Joseph and Mary, and that a separate supernatural being, the Christ, came upon Jesus at his baptism and departed at his crucifixion. According to the third century bishop Dionysius of Alexandria, “the doctrine he taught was this: that the kingdom of Christ will be an earthly one.” Cerinthus “was himself devoted to the pleasures of the body and altogether sensual in his nature.” In Dionysius’ day, some claimed that Cerinthus wrote the book of Revelation

Monday, November 11, 2013

YALIYO JILI KWENYE IBADA YA PAMOJA (JOINT-MASS) ILIYO ANDALIWA NA CASFETA TAWI LA UHASIBU SINGIDA

HAWA NI BAADHI TU YA WANA CASFETA TAWI LA UHASIBU
Mama Wema akihubiri kwenye ibada ya pamoja
Wana CASFETA wakimchezea Mungu kwenye sifa katika ibada ya pamoja
Mchungaji Mlezi wa CASFETA tawi la Uhasibu Abeli Manupa akiwaombea wanafunzi
Mwenyekiti wa CASFETA tawi la Uhasibu akimkaribisha Mchungaji Abeli Manupa
Wana CASFETA wakiwa wamezama kwenye Maombi
Mwenyekiti wa Maombi CASFETA uhasibu akisikiliza neno
Mwimbaj wa nyimbo za injili mkoani Singida Miriam Mushi akiwasalimia wana CASFETA
Hao ni wana CASFETA toka Mwenge High School wakimwimbia Bwana
Mwenyekiti wa CASFETA manispaa akitoa matangazo yanayohusu Kongamano la CASFETA TAIFA
Praise and worship team wakimsifu Mungu kwenye ibada ya pamoja (JOINT MASS)
Mwimbaji wa nyimbo za injili Gilbert Godfrey akimtumikia Mungu kwa uimbaji
Praise and worship team wakienda sawa kwenye Joint mass

Wednesday, November 6, 2013

JINSI ILIVYOKUWA KWENYE MKESHA WA MAOMBI ULIO FANYIKA TAREHE 18-10-2013

Mwenyekiti wa HUIMA tawi la UHASIBU akiwasalimia wanafunzi waliohudhuria kwenye mkesha

Katikati ni katibu wa CASFETA Mr. Bryson Mollel akiwa na wataalam wa muziki kwenye mkesha!1
Wana CASFETA wakiwa kwenye maombi
Mchungaji Abel Manupa akiwaombea wana CASFETA kwenye mkesha wamaombi ulio andaliwa na  CASFETA na HUIMA
Wana CASFETA wakisikiliza neno la MUNGU lililokuwa likihubiri wa  Mchu Abel Manupa kwenye mkesha!
Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya kikristo UVVKT Raphael Lalashe akiwasalimia wapendwa kwenye mkesha
Timu ya kusifu na kuabudu wakimwimbia BWANA kwenye mkesha wa maombi uliofanyika tarehe 18-10-2013
Mr. Frank A. Kasanga mwenyekiti wa CASFETA akiwa na Mwenyekiti wa HUIMA kwenye mkesha wa maombi uliofanyika Ijumaa ya tarehe 18-10-2013, wakiwasalimia wana CASFETA na HUIMA

Sunday, October 13, 2013

Ninawezaje kushinda dhambi katika maisha yangu ya kikristo?

Biblia inazungumzia juu ya vitu hivi tulivyonavyo ili tushinde maisha yetu ya dhambi:

(1) Roho Mtakatifu – kipawa kimojachapo ambacho Mungu ametupa (kanisa lake) kwa ajili ya kuwa na ushindi katika maisha ya kikristo ndani ya Roho Mtakatifu. Mungu anatofautisha mtendo ya mwili na matunda ya Roho Mtakatifu katika wagalatia 5:16-25. katika andiko hilo tunashauriwa kutembea katika uwepo wa Roho Mtakatifu. “waumini wote tayari wamejazwa na Roho Mtakatifu”,lakini hapa tunasisitizwa kupatia nafasi Roho Mtakatifu atutawale na kutuongoza. Hii ina maana ya kuwa tusikilize sauti yake tusije tukatenda mapenzi yetu wenyewe.

Tofauti ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuifanya maishani mwa mtu ni kama ile ya Petro, kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mara tatu, na alikuwa mbeleni ameahidi kumfuata Yesu mpaka kwenye hatari ya kifo angekufa naye. Baada ya kujazwa na Roho alizungumza waziwazi na kwa ujasiri mbele ya wayahudi juu ya mwokozi katika siku ya pentekote.

Unatembea ndani ya Roho ukiwa humzuii anapotaka kujidhihirisha (“kumzima Roho” wathesalonike wa kwanza 5:19) na una kiu ya kujazwa naye kila wakati (Waefeso 5:18-21). Je mtu hujazwaje na Roho Mtakatifu? Kwanza ni kwa mapenzi ya Mungu kama vile ilivyo katika agano la kale. Alikuwa akichagua watu Fulani, kuwajaza kwa ajili ya kutekeleza kazi ama wadhifa Fulani (Mwanzo 41: 38; Kutoka 31:3; Hesabu 24:2; Samueli wa kwanza 10:10; na kadhalika.) Ninaamini kuwa kuna ushahidi katika Waefeso 5:18-21 na Wakolosai 3:16 yakuwa Mungu huchagua kujaza wale wanaojijaza Neno la Mungu kwa kuwa kote kote ni kujazwa uwezo wa Mungu.

(2) Neno la Mungu, Biblia – Timotheo wa pili 3:16-17 inasema ya kwamba Mungu ametupa neno lake ili lituandae katika kufanya kazi njema. Linatufundisha jinsi ya kuishi na cha kuamini, linatufunulia kama tumetenda makosa na kuturudisha katika njia ya sawa. Kama waebrania 4:12 inavyosema Neno la Mungu liko hai na lina nguvu ya kupenya ndani ya nafsi zetu kung’oa lile tatizo ambalo mwanadamu hangeweza kulitatua. Mwandishi wa zaburi azungumzia uwezo wa Neno la Mungu juu ya kubadilisha maisha ya watu katika zaburi 119:9,11,105 na aya nyengine. Joshua aliambiwa siri ya kushinda adui zake (inayoashiria pia vita vyetu vya kiroho) ni kwamba asilisahau Neno la Mungu bali alitafakari usiku na mchana ili akalitimize. Haya aliyatenda, ijapokuwa maagizo yenyewe hayakuwa na uhusiano na mambo ya kivita lakini yakampa ushindi katika vita vya kuimiliki nchi ya ahadi.

Hii ni sehemu ambayo mara nyingi tunaipuuza. Tunapenda kubeba biblia tukienda kanisani ama kusoma aya za kukariri lakini hatuyatilii maanani yale tuyasomayo. Hatuyatafutii nafasi maishani mwetu kiasi cha kutubu dhambi zetu na kumtukuza Mungu kwa kipawa hiki. Tunasoma tu kiasi cha kupata mtazamo Fulani juu ya wokovu lakini hatuongezi juhudi zozote katika kutafakari kwetu mara kwa mara kiasi cha kutufanya tuwe na afya nzuri kiroho.

Ni muhimu sana kwako ufanye tabia ya kusoma neno la Mungu. Kama bado hujazoea basi Roho anakusisitiza uwe na tabia ya kulisoma Neno la Mungu. Nina kushauri uwe na kumbukumbu ya yale uliyoyasoma kwa kuyanakili kwenye daftari lako au kwenye kompyuta. Biblia ndicho kifaa Roho hutumia katika maisha yetu na maisha yaw engine (Waefeso 6:17), ikiwa ni sehemu kubwa ya silaha mojawapo ambayo Mungu hutupa ili tupigane vita vya kiroho (Waefeso 6:12-18)!

(3) Maombi – Hii pia ni njia nyengine ambayo Mungu ametupatia. Njia hii wakristo wengi huitaja tu kwa maneno lakini hawaitumii. Tuna ibada za maombi na nyakati za maombi na kadhalika lakini hatuoni manufaa ya jambo hilo sawa na kanisa la kwanza (Matendo 3:1; 4:31; 6:4; 13:1-3, na kadhalika). Paulo mara kwa mara arudia kueleza vile alikuwa akiwaombea wale aliokuwa akiwahudumia. Lakini tunapokuwa peke yetu hatuitumii njiaa hii. Mungu ametuahidi mambo mazuri ya ajabu kuhusiana na maombi (Mathayo 7:7-11; Luka 18:1-8; Yohana 6:23-27; Yohana wa kwanza 5:14-15, na kadhalika.) Paulo analiongezea mkazo tena katika mafundisho yake juu ya kujiandaa kwa ajili ya vita vya kiroho (Waefeso 6:18)!

Je, ni muhimu kiasi gani njia hii? Tunapomtazama tena Petro, tunaona maneno ya kristo aliyomwambia kabla hajamkana kule Gethsemane. Yesu alipokuwa akiomba Petro alilala. Yesu akamwambia, “Kesheni mkiomba ili msiingie majaribuni: Roho inataka lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41). Wewe pia kama Petro unataka kufanya mema lakini huna nguvu yakutosha kufanyia hayo. Lazima tufuate mausia ya Mungu, tuendelee kumtafuta, tukibisha na kumuuliza… na atatupatia nguvu ile tuitafutayo (Mathayo 7:7 na kuendelea). Lakini lazima tuitilie mkazo njia hii maishani mwetu ndiyo tufaulu. Sisemi ya kwamba maombi ndiyo njia maalum zaidi. La sivyo. Mungu ni wakutisha. Maombi ni kukubali hali zetu za udhaifu, ukuu wa Mungu mwenye nguvu na asiyeshindwa ili tupate uwezo huo huo tuweze kuyafanya yaliyo mapenzi yake (wala si yetu) (Yohana wa kwanza 5:14-15).

(4) Kanisa – Hii ni mojawapo ya njia tunazozifumbia jicho. Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili (Mathayo 10:1). Tunaposoma juu ya habari za safari za wale wamishenari katika kitabu cha matendo ya mitume, hawakuenda mmoja mmoja bali katika makundi, wawili wawili au zaidi.Yesu alisema mahali wawili au watatu wamekusanyika kwa ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao (Mathayo 18:20). Anatuamuru tusiache kukusanyana pamoja kama kawaida za watu wengine zilivyo bali tuutumie wakati wa kuwa pamoja kwetu kwa kutiana moyo katika upendo na matendo mema (Waebrania 110:24-25). Anatuagiza kutubu dhambi zetu mmoja kwa mwingine (Yakobo 5:16). Katika habari za hekima katika agano la kale tunaambiwa ya kwamba chuma hunoa chuma mwenziwe, vivyo hivyo mtu huchangamsha sura ya rafiki yake (Methali 27:17) “kamba ya nyuzi tatu haikatiki rahisi.” “kuna nguvu katika umoja wa wengi (Mhubiri 4:11-12).

Baadhi ya watu ninaowafahamu wamepata kaka na dada katika kristo wanaotangamana pamoja au kwa simu na wanaelezana vile wanaendelea na maisha ndani ya kristo na wanawajibika katika kuombeana huku wakiishi maisha sawa na Neno la Mungu. Mabadiliko mara nyingine huja haraka na wakati mwengine polepole. Lakini Mungu ametuahidi ya kwamba kadri tunavyoendelea kutumia njia hizi alizotuwekea, ndivyo atatuletea mabadiliko maishani mwetu. Vumilia ukijua ya kuwa ni mwaminifu katika ahadi zake.